Aliambiwa ananuka kama mbuzi, sasa awaonyesha yeye ni simba, tazama alivyofanya.......
Gavana Mvurya aungana na kina mama kucheza ngoma ya kitamaduni katika mojawapo wa hafla katika kauti ya Kwale Imetolewa: www.standardmedia.co.ke Gavana wa Kwale SalimMvury a ana sababu za kushangilia baada ya Kaunti ya Kwale kutajwa kama mojawapo wa kaunti ambazo zinatumia pesa za miradi ya maendeleo kwa njia sawasawa. Taarifa katika gazeti la Nation zinasema Kaunti ya Kwale ilitumia asilimia 57.3 ya matumizi yake ya maendeleo, hiki kikiwa ndicho kiwango cha juu zaidi cha matumizi katika mwaka wa serikali ulioisha Juni 30. Zamani, Mvurya alikuwa afisa wa maendeleo ya kijamii akifanya kazi na shirika la Plan International na huenda hapo ndipo alikereka na umaskini mkubwa ulioenea katika eneo la Kwale. Alipochaguliwa Mvurya aliyapatia kipaumbele maswala ya kuimarisha jamii kama vile kutengeneza barabara, maji na elimu na kutenga zaidi ya shilingi Milioni 400 kwa miradi hiyo. Taarifa hizo bila shaka huenda zikaweka kicheko cha ushindi katika mid...